Suivant

Bima ya afya ya jamii kusaidia wanafunzi

13/03/24
K24 TV
Dans Afrique / Kenya

Wanafunzi wa shule za umma kuanzia chekechea hadi sekondari sasa watanufaika na mpango wa matibabu chini ya bima ya afya ya jamii (SHIF). Akiwasilisha majibu yake mbele ya kamati ya elimu ya bunge, katibu mkuu wa elimu, belio kipsang pia amtetea serikali kuwa ijapokuwa ilitamatisha utumizi wa edu afya, bado wanaendelea kuwapa matibabu wanafunzi 4 walioko india. Suala hilo liliibuka baada ya wanafunzi walioko chini ya mpango wa edu afya kuwasilishiwa barua novemba mwaka jana ya kutamatika kwa mpango huo bila ya kuwa na mpango mbadala.

Montre plus

 0 commentaires sort   Trier par


Suivant