التالي

Madaktari katika hospitali ya mafunzo na rufaa ya Moi wafanya maandamano katika mji wa Eldoret

21/03/24
K24 TV

Madaktari katika hospitali ya mafunzo na rufaa ya Moi wamefanya maandamano katika mji wa Eldoret kwa muda wa saa nne kuendelea kuishinikiza wizara ya afya kushughulikia matakwa yao. Wakiongozwa na maafisa wa muungano wa KMPDU kutoka eneo hilo, madaktari hao walioandama pamoja na wanafunzi wa utabibu walimshtumu vikali waziri wa afya Susan Nakhumicha kwa kile walichodai ni kudharauliwa kwa kada yao.

أظهر المزيد

 0 تعليقات sort   ترتيب حسب


التالي