下一个

Jenerali Francis Ogolla aeenziwa kama mtu aliyejitolea

20/04/24
K24 TV
非洲

Jenerali Francis Ogolla ameenziwa kama mtu aliyejitolea ,aliyependa taifa na kazi yake na mnyenyekevu. Wakizungumza wakati wa hafla ya kijeshi ya kumpa heshima zake za mwisho, wengi wamemtaja kama mtu aliyeishi maisha ya kupigiwa mfano, asiyetaka makuu na mwenye bidii. Rais William Ruto ameahidi kuanzisha mikakati ya kununua vifaa vya kisasa vya kijeshi ili kuepuka mikasa kama uliopelekea kifo cha Ogolla na maafisa wengine wa KDF. Kinara wa Azimio Raila Odinga hata hivyo ametaka uchunguzi wa kina cha mkasa kufanyika mara moja ,akimtaja mwendazake kama shujaa wa taifa.

显示更多

 0 注释 sort   排序方式


下一个