下一个

Watu sita wafariki kutokana na maporomoko ya ardhi Murang'a

29/04/24
K24 TV
非洲

Wizara ya usalama wa ndani imetoa onyo kali kwa wakenya wanaokiuka tahadhiri za mafuriko yanayoshuhudiwa nchini na kuhatarisha maisha ya wakenya wengine. Kupitia taarifa iliyochapishwa rasmi hii leo na kutiwa sahihi na waziri Kithure Kindiki, wale watakaopatikana wakivuka mito iliyofurika au kuvusha watu kwa mashua watakamatwa na kufunguliwa mashtaka tofauti. Haya yanawadia huku watu sita wakiripotiwa kufariki kaunti ya murang’a baada ya kuhusika katika mkasa wa maporomoko ya ardhi.

显示更多

 0 注释 sort   排序方式


下一个