Suivant

SEKTA YA AFYA YAZIDI KUIMARIKA BABATI

19/03/24
CLOUDSMEDIA
Dans Afrique / Tanzanie

HOSPITALI YA HALMASHAURI YA MJI BABATI Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT  Samia Suluhu Hassan imekamilisha ujenzi wa majengo mapya na miundombinu ya hospitali  ya Mji Babati kwa zaidi ya shilingi milioni 500 likiwemo jengo la huduma ya Mama na Mtoto  na jengo la dharula. Tangu enzi na enzi hapa Babati hapakuwahi kuwa na hospitali inayotoa huduma za rufaa, wagonjwa walisafirishwa umbali wa zaidi ya 200km hadi Dodoma na mara kadhaa wapo walioshindwa kumudu gharama za usafiri. Daktari Kyabatoli anaripoti kuwa hospitali hii imeanzishwa tangu mwaka 1958 na kupanda  hadhi taratibu na sasa tayari Se rikali imetoa bil 1.4 kwaajili ya ujenzi wa majengo mengine.

Montre plus

 0 commentaires sort   Trier par


Suivant